• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la UM lazitaka pande mbalimbali nchini Mali kutekeleza makubaliano ya amani

    (GMT+08:00) 2020-01-18 19:27:12

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limezitaka pande mbalimbali nchini Mali kuonesha dhamira za kisiasa ili kuharakisha utekelezaji wa makubaliano yao kuhusu amani na maafikiano yaliyofikiwa mwaka 2015.

    Kwenye taarifa yao kwa vyombo vya habari, nchi wajumbe wa Baraza la Usalama wameeleza maendeleo kadhaa yaliyopatikana katika utekelezaji wa makubaliano hayo lakini pia wameonesha wasiwasi mkubwa kuhusu kuchelewa kwa utekelezaji wa vifungu vingi muhimu kwenye makubaliano hayo.

    Hata hivyo baraza hilo limetiwa moyo kwa kuanza kupelekwa tena kwa vikosi vya kwanza vya jeshi la Mali lililoundwa na kupangwa upya kwenye sehemu ya kaskazini ya nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako