• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yamwekea vikwazo jenerali wa jeshi la Iran

    (GMT+08:00) 2020-01-19 16:44:38

    Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imemwekea vikwazo brigedia jenerali Hassan Shahvarpour wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC ambaye ni kamanda wa jeshi hilo mkoani Khuzestan.

    Wizara hiyo imemkosoa kwa kuongoza jeshi kuwaua waandamanaji wa Iran mwezi Novemba mwaka jana. Kwa mujibu wa vikwazo hivyo, brigedia jenerali Hassan Shahvarpour na wanafamilia wake wa karibu hawataruhusiwa kuingia nchini Marekani.

    Uamuzi huo umekuja wakati wa mivutano mikubwa kati ya Marekani na Iran kufuatia Marekani kumwua kamanda mkuu wa jeshi la Iran na shambulizi la makombora la Iran dhidi ya kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq.

    Habari nyingine zinasema waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amefuta uwezekano wa kufanya mazungumzo yoyote kuhusu makubaliano mapya ya nyuklia. Bw. Zarif alisema hayo Ijumaa kwenye ziara yake mjini Mumbai, India kuhudhuria mkutano ulioongozwa na Shirikisho la Wenye Viwanda la India, ambapo pia alitoa wito kwa serikali ya India kuishawishi serikali ya Marekani irudi kwenye makubaliano hayo iliyojitoa mwaka 2018 kufuatia uamuzi wa rais Donald Trump.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako