• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China apongeza mwanzo mzuri wa mambo ya diplomasia ya China mwaka 2020

    (GMT+08:00) 2020-01-19 16:45:39

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ameipongeza ziara ya rais Xi Jinping wa China nchini Myanmar kuwa ni mwanzo mzuri wa shughuli za kidiplomasia za China kwa mwaka 2020.

    Bw. Wang amewaambia wanahabari hayo baada ya kumalizika kwa ziara ya siku mbili ya rais Xi nchini Myanmar, akieleza kuwa rais Xi ameshiriki kwenye shughuli 12 na kushuhudia kusainiwa kwa nyaraka 29 za ushirikiano katika nyanja mbalimbali katika mji mkuu wa nchi hiyo Nay Pyi Taw.

    Amesema hii ilikuwa ziara ya kwanza ya rais Xi nje ya nchi kwa mwaka huu pia hatua muhimu ya kidiplomasia iliyofanywa na China kwa nchi yake jirani. Amesisitiza urafiki wa kindugu kati ya China na Myanmar ulioonyeshwa wakati wa ziara hiyo pamoja na makubaliano mengi yaliyofikiwa na pande hizo mbili.

    Bw. Wang amesema kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa Jumamosi, China na Myanmar zimekubaliana kushirikiana kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja na kufungua ukurasa mpya wa uhusiano wa pande mbili. Na uamuzi huo utaendelea kuingiza nguvu mpya ya uhai na uchangamfu kwenye ushirikiano wa nchi hizo mbili.

    Ili kuadhimisha miaka 70 ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi, nchi hizo mbili zimeamua kuzindua Mwaka wa Utamaduni na Utalii kati yao na kufanya shughuli zaidi ya 70, ambazo zitaongeza kuelewana na kuaminiana kati ya watu wa nchi hizo mbili.

    Bw. Wang amesema rais Xi amefikia makubaliano mapya muhimu na viongozi wa Myanmar kuhusu ushirikiano bora chini ya pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kwamba mradi wa Ushoroba wa Kiuchumi kati ya China na Myanmar utaingia kwenye kipindi cha ujenzi halisi kutoka wazo tu.

    Bw. Wang pia amepongeza miongo ya juhudi za pamoja za China na Myanmar ili kushikilia Kanuni Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani: kuheshimiana kwa mamlaka na ukamilifu wa ardhi, kutovamiana, kutoingilia mambo ya ndani ya kila upande, usawa na kunufaishana pamoja na kuishi pamoja kwa amani.

    Bw. Wang ameeleza kuwa wakati vitendo vya kujilinda kibiashara, kufanya maamuzi ya upande mmoja na umwamba vinaendelea kuvuruga mahusiano ya kimataifa, China na Myanmar zina changamoto mpya katika kulinda mamlaka, usalama, na maslahi ya maendeleo, kwa hivyo kuelewana na kuungana mkono ni muhimu kwa nchi hizo mbili.

    Kwenye ziara yake Rais Xi alikutana na mwenzake wa Myanmar Bw. U Win Myint, mshauri mkuu wa serikali Bibi Aung San Suu Kyi na kamanda mkuu wa vikosi vya ulinzi Bw. Min Aung Hlaing. Hii ni ziara ya kwanza kwa rais wa China nchini Myanmar baada ya miaka 19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako