• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya wanasheria wa Rais Trump yawalaani wabunge wa chama cha Democrats kwa hatua ya kumshitaki Rais

    (GMT+08:00) 2020-01-19 17:05:08

    Timu ya wanasheria ya ikulu ya Marekani imezilaani juhudi za baraza la wawakilishi za kumshtaki rais Trump, na kuitaja hatua hiyo kuwa ya "kutia aibu, kinyume cha sheria, na inajaribu kubadilisha matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2016.

    Jana wajumbe wa Democrats wa baraza la wawakilishi la bunge la Marekani waliwasilisha hoja yao ya kisheria dhidi ya rais Trump kwenye kurasa 111 kwenye baraza la seneti, wakimshitaki Rais huyo kwa kutumia vibaya madaraka na kuzuia utendaji wa bunge, hivyo wanataka aondolewe madarakani. Wawakilishi hao wanaona ushahidi unaonyesha wazi kuwa rais Trump ana hatua ya yote mawili, lakini pia wamesema ni jukumu la baraza la seneti kutekeleza wajibu wao. Usikilizaji wa hoja hiyo utaanza jumanne chini ya jaji mkuu John Roberts.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako