• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa IMF amesema makubaliano ya biashara kati ya China na Marekani yanapunguza sintofahamu duniani

    (GMT+08:00) 2020-01-19 17:05:31

    Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF Bibi Kristina Georgieva, amesema makubaliano ya biashara ya hatua ya kwanza yaliyosainiwa hivi karibuni kati ya China na Marekani yamepunguza sintofahamu iliyokuwa inakwamisha ongezeko la uchumi duniani.

    Akiongea mjini Washington kwenye mkutano wa jumuiya ya washauri bingwa, Bibi Georgieva amepongeza makubaliano hayo na kusema IMF itafanya makadirio ambayo inatarajia kuyatoa kesho jumatatu ikiwa ni mtazamo wa mwelekeo ya uchumi wa dunia, utakaotolewa kwenye mkutano wa baraza la uchumi wa dunia utakaofanyika mjini Davos.

    Amesema kusainiwa kwa makubaliano hayo, kutafanya ongezeko la uchumi wa China kwa mwaka huu kufikia asilimia sita, na sio chini ya hapo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako