• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chama tawala cha Tanzania chaonya kuhusu kutaja majina ya wagombea uchaguzi mwaka 2020

    (GMT+08:00) 2020-01-20 08:58:29

    Makamu mwenyekiti wa chama tawala cha Tanzania CCM Bw. Philip Mangula, amewaonya wanachama wa chama cha mapinduzi kutofichua majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

    Akiongea kwenye mkutano wa jumuiya ya wanawake mjini Dodoma, amesema maamuzi kuhusu majina ya wagombea yanatakiwa kuwa siri hadi yatakapotangazwa, na kuonya kuwa watakaofichua majina hayo wataadhibiwa.

    Bw. Mangula amezitaka jumuiya za chama ikiwa ni pamoja na jumuiya ya wanawake, kuanza kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao ambao chama cha mapinduzi kinatarajia kupata ushindi mkubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako