• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkali wa MMA, Conor McGregory aandika historia kwa kumtangwa Donald Cerrone ndani ya sekunde 40

    (GMT+08:00) 2020-01-20 09:17:45

    Mkali wa MMA, Conor McGregory ameandika historia mpya katika maisha yake ya ulingoni baada ya kumpiga mpinzani wake, Donald Cerrone kwa TKO raundi ya kwanza tu ndani ya sekunde 40 na kujikuta akibubujikwa na machozi mara baada ya ushindi huo. Katika pambano hilo lililomrudisha rasmi, Conor McGregory katika ulimwengu wa 'Mixed martial arts' (MMA) mchezo ambao unaruhusu kutumia viungo vyote vya mwili, lilimshuhudia bingwa huyo wa MMA akionyesha uwezo wa hali ya juu. Pambano hilo lisilo la ubingwa limepigwa T-Mobile Arena huko Las Vegas. McGregor sasa ni bondia wa kwanza kushinda kwa KO kwenye uzito wa Featherweight, Lightweight na Welterweight.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako