• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • GDP kwa kila mtu China yazidi dola za kimarekani elfu kumi

    (GMT+08:00) 2020-01-20 10:03:59

    Msemaji wa Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bibi Meng Wei amesema, mwaka 2019 wastani wa pato la taifa la China kwa kila mtu umezidi dola za kimarekani elfu kumi, hali ambayo imeonesha kuwa nguvu ya jumla na tija ya kijamii ya China vimeongezeka, kiwango cha maisha ya wananchi kimeinuka, na China imepiga hatua madhubuti katika njia ya kuelekea kuwa nchi yenye pato la juu duniani. Hayo ni mafanikio makubwa iliyopata China katika kujenga jamii yenye maisha bora. Lakini Bw. Meng Wei pia ameeleza kuwa wastani wa pato la taifa kwa kila mtu katika nchi zilizoendelea umezidi dola za kimarekani elfu 30, hivyo China bado ni nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako