• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi afanya ziara ya ukaguzi mkoa wa Yunan

  (GMT+08:00) 2020-01-20 10:16:14

  Rais Xi Jinping wa China yuko ziarani mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China katika ziara ya ukaguzi kabla ya mwaka mpya wa jadi wa kichina.

  Rais Xi ameenda kijiji cha kabila la Wa kilichoko kwenye wilaya ya Qingshui mjini Tengchong, ili kufahamu kuhusu kazi ya kuondokana na umaskini, huku akitoa salamu za mwaka mpya wa jadi kwa wanakijiji.

  Pia ametembelea mji wa kale wa Heshun, ambao ulikuwa lango la Njia Hariri ya Kale ya Kusini iliyounganisha Sichuan, Yunnan na Myanmar na India, ili kufahamu zaidi kuhusu mawasiliano, urithi wa kihistoria na kiutamaduni pamoja na hifadhi ya kiikolojia na kimazingira kwenye njia hiyo ya kibiashara.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako