• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watuhumiwa milioni 1.81 wa uhalifu washatkiwa nchini China kwa mwaka 2019

  (GMT+08:00) 2020-01-20 10:16:38

  Mkutano wa wakuu Idara za waendesha mashtaka uliofanyika Beijing wikiendi hii, umesema watuhumiwa zaidi ya milioni 1.81 walikamatwa na kufikishwa mahakamani mwaka 2019.

  Mwaka jana watuhumiwa wapatao elfu 90 wameshtakiwa kutokana na uhalifu wa mtindo wa mafia, ambayo imeongezeka kwa asilimia 60.3 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia. Watuhumiwa zaidi ya elfu 1.4 wameshtakiwa kutokana na kutoa ulinzi kwa uhalifu kama huo.

  Idara kuu ya mashtaka ya China imefikia makubaliano na wizara ya usalama wa umma ili kuingilia kati mapema kesi zote za uhalifu wa kupangwa wenye mtindo wa mafia kuanzia mwaka huu.

  Mwaka 2018 China ilizindua kampeni dhidi ya uhalifu wa kupangwa na maofisa wanaoyalinda makundi ya uhalifu, ili kuhakikisha usalama wa jamii na kuboresha hisia ya wananchi kujitimiza, furaha na usalama.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako