• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaendelea kuwa makini kutokana na kesi mpya za nimonia kuripotiwa

  (GMT+08:00) 2020-01-20 17:04:01

  Miji zaidi ya nchini China imeongeza usimamizi, udhibiti, na kinga ya magonjwa yanayotokana na mfumo wa hewa baada ya kuongezeka kwa kesi zaidi zinazohusishwa na ugonjwa wa nimonia.

  Mji wa Wuhan ulioko katikati ya China, ambako kesi ya kwanza ya maambukizi ya virusi kwenye mfumo wa hewa (2019-nCoV) kugunduliwa, umethibirisha kuwa mtu wa tatu amefariki kutokana na ugonjwa huo. Mamlaka ya mji huo zimesema, jumla ya kesi mpya 136 ziliripotiwa katika mji huo kati ya jumamosi na jumapili. Kamati ya Afya ya Manispaa ya Wuhan imesema, wagonjwa hao walionyesha dalili kama vile homa, kukohoa, ama maumivu ya kifua kabla ya Jumamosi iliyopita.

  Kesi mpya tatu za ugonjwa huo, mbili mjini Beijing na moja huko Shenzhen, ziliripotiwa, ikiwa ni mara ya kwanza kwa ugonjwa huo kugunduliwa nje ya mkoa wa Wuhan. Wagonjwa wote hao watatu walikuwa Wuhan hivi karibuni.

  Taasisi za afya nchini China zinafuatilia kwa makini maendeleo ya ugonjwa huo wakati msongamano wa safari katika kipindi cha Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina ukiendelea.

  Kamati ya Afya ya Taifa imesema, imeunda mfumo wa kila siku wa kitaifa unaotoa ripoti za masuala ya afya, na kutoka vifaa vya kuchukua vipimo ili kuimarisha ufuatiliaji. Vilevile, Kamati hiyo imesema, inapaswa kuongeza ushirikiano na mawasiliano ya kimataifa, kubadilishana habari kwa wakati na Shirika la Afya Duniani WHO, na maeneo ya Hong Kong, Macao na Taiwan ya China na nchi husika kuhusu kuenea kwa ugonjwa huo, na kupashana habari kuhusu utaratibu wa muundo wa jini za virusi.

  Mpaka kufikia saa nne usiku wa jana, jumla ya kesi 198 za nimonia ziliripotiwa mkoani Wuhan, na kesi 25 kati ya hizo, wagonjwa wametibiwa na kuruhusiwa kuondoka hospitali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako