• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mwanasoka nguli wa Kenya Dennis Oliech, astaafu soka

    (GMT+08:00) 2020-01-20 18:17:14

    Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Harambee Stars ya Kenya Dennis Oliech, amestaafu rasmi soka. Oliech, ambaye alikuwa anadaiwa kuwa na matumaini ya kujiunga na klabu nyingine ya Ligi Kuu ya Kenya (KPL), aliichezea Gor Mahia mara ya mwisho baada ya kujiunga nao Januari, 2, 2019. Oliech aliamua kusitisha kusakata kabumbu baada ya kushindwa kupata klabu nyingine ya KPL kumsajili na sasa ameamua kufanya biashara. Oliech pia anaripotiwa kutaja changamoto za kifedha katika vilabu vya Kenya kama chanzo chake kustaafu. Oliech, ambaye ndiye fundi bora wa mabao wa Harambee Stars pia alidokezea kuanzisha kampuni ya kuwasaidia wanasoka chipukizi kuvichezea vilabu vya Ulaya. Mchezaji huyo mwenye miaka 34, anaaminika kuwa na mkataba wa miaka miwili na K'Ogalo katika ofa ambayo ilimshuhudia akiwa mchezaji aliyekuwa akilipwa zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako