• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazingatia zaidi maeneo yenye umaskini zaidi katika vita yake dhidi ya umaskini

    (GMT+08:00) 2020-01-20 18:58:19

    China imepanga kuchukua hatua mbalimbali kutatua matatizo yanayoyakabili maeneo yenye kiwango cha juu cha umaskini ili kuzuia watu walioondolewa umaskini kuwa maskini tena, ikiwa huu ni mwaka wa mwisho wa China kuondokana na umaskini.

    Hivi sasa, ingawa idadi ya watu maskini wanaoishi katika maeneo yenye umaskini uliokithiri imepungua, lakini maeneo hayo yanakabiliwa na matatizo mengi ya kimaendeleo, ikiwemo, hali duni ya miundombinu, na huduma za umma.

    Aidha, kuhusu watu maskini wapya na watu waliorejea kuwa maskini, serikali inapaswa kuhakikisha utekelezaji wa hatua na sera zilizopo, kuvumbua hatua zenye ufanisi ili kuhakikisha mafanikio ya kuondoa umaskini.

    Habari zinasema, idadi ya watu maskini vijijini nchini China imepungua kutoka milioni 98.99 ya mwaka 2012 hadi milioni 6 ya mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako