• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • CMG yafanya mkutano na wanahabari kuhusu tamasha la Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina

  (GMT+08:00) 2020-01-20 19:04:01

  Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG limefanya mkutano na wanahabari kuhusu tamasha la sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina ambalo hufanyika wakati wa mkesha wa sikukuu hiyo.

  Mwaka huu, tamasha hilo litakuwa na mambo kadhaa ikiwemo ngonjera, nyimbo, ngoma, opera, viinimacho, na sarakasi, litakuwa na uvumbuzi wa aina mbalimbali. Pamoja na Beijing, tamasha hilo pia litakuwa na majukwaa mkoani Henan na katika sehemu ya ghuba kubwa ya Guangdong, Hong Kong na Macao.

  Licha ya vyombo vya CMG na mashirika ya utangazaji ya China katika ngazi mbalimbali, vyombo vya habari zaidi ya 50 vya nchi na sehemu zaidi ya 170 duniani ikiwemo Marekani, Uingereza, Japan, Russia, Brazil, Singapore, Falme za Kiarabu, Malaysia, Thailanda na Laos pia vitatangaza moja kwa moja tamasha hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako