• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China asisitiza kuzingatia zaidi maisha na afya ya wananchi kutokana na ugonjwa wa nimonia

  (GMT+08:00) 2020-01-20 20:05:41

  Rais Xi Jinping wa China amesema, hivi karibuni kesi za aina mpya za nimonia zimeripotiwa kwa mfululizo katika sehemu kadhaa haswa mji wa Wuhan, na kuzitaka idara husika kutilia maanani hali hiyo, pia kufanya vizuri kazi ya kukinga na kudhibiti ugonjwa huo kwa nguvu zote.

  Rais Xi amesema hivi sasa watu wanasafiri kwa wingi kutokana na sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina, hivyo idara husika za chama na serikali zinapaswa kuzingatia zaidi maisha na afya ya wananchi, na kuchukua hatua madhubuti kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.

  Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang pia ametoa maagizo kuhusu za kukabiliana na ugonjwa huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako