• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uhaba wa nyanya waendelea kushuhudiwa bei ikipanda

    (GMT+08:00) 2020-01-20 20:39:25

    UHABA wa nyanya umeshuhudiwa maeneo mbalimbali nchini kufuatia mvua inayoendelea kunyesha.

    Bei ya nyanya mwezi huu wa Januari imepanda ikilinganishwa na miezi mingine.

    jiji la Nairobi, kifungu cha nyanya tatu kinauzwa Sh25.

    kreti ya kilo 90 sasa inagharimu kati ya Sh7, 000 – 7, 500, kipimo hicho, nyanya zikiwa nyingi, hukinunua kati ya Sh2, 000 – 2, 500, kikiwa ghali hakipiti Sh3, 500.

    Watalaamu wa masuala ya kilimo wanahimiza wakulima kukuza mbegu zinazoweza kustahimili changamoto za wadudu na magonjwa yanayosababishwa na maji.

    Wakulima pia wanashauri kuzingatia muundo wa shamba, wakihimizwa kupanda nyanya eneo lililoinama kiasi ili kuepushia zao hilo athari za maji.

    Isitoshe, kutokana na ughali wa bidhaa hiyo hasa wakati huu kiwango cha uchumi kinazidi kuwa ghali, watu wanashauriwa kutumia viungo mbadala kama vile pilipili mboga, karoti, kuongeza mlo ladha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako