• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bidco Africa yashirikiana na wanawake kibiashara

  (GMT+08:00) 2020-01-20 20:39:44

  KAMPUNI ya Bidco Africa Ltd imetia saini mkataba baina yake na wafanyabiashara wanawake kutoka tabaka tofauti kwa minajili ya ushirikiano.

  Wafanyabiashara kutoka sekta tofauti wapatao 100 wakutana katika makao ya kampuni ya Bidco Africa mjini Thika ili kutafuta mbinu mwafaka jinsi ya kujipanua kibiashara.

  Hafla hiyo ya siku moja ilijumuisha wanawake kutoka jijini Nairobi na miji mingine huku lengo lao kuu likiwa kupata ushauri zaidi jinsi ya kupanua biashara na kujitegemea kwa njia ya kipekee.

  Mwenyeki wa kampuni hiyo na pia mmiliki wake Dkt Vimal Shah alikuwa mstari wa mbele kuwahamasisha kuhusu hali ya biashara na jinsi ya kusalia kwenye sekta hiyo kwa muda mrefu.

  Aidha amesema yeye kama gwiji wa biashara kwa muda mrefu atashirikiana na wao kwa kuwapelekea biadhaa za Bidco Afrika katika makazi zao ili wauzie wateja sehemu hizo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako