• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yathibitisha maambukizi kati ya mtu na mtu kwa virusi vipya vya nimonia aina ya 2019-nCoV

  (GMT+08:00) 2020-01-21 09:27:38

  Timu ya wataalamu kutoka Kamisheni ya Afya ya Taifa ya China imethibitisha maambukizi kati ya mtu na mtu kwa virusi vipya vya nimonia aina ya 2019-nCoV.

  Kiongozi wa timu hiyo mwanaakademia Zhong Nanshan amesema maambukizi mawili yaliyoripotiwa mkoani Guangdong yamethibitishwa kuwa ni maambukizi kati ya mtu na mtu. Pia amethibitisha kuwa baadhi ya wafanyakazi wa afya pia wameambukizwa virusi hivyo.

  Virusi hivyo viligunduliwa mara ya kwanza katika mji wa kati wa Wuhan, ambako mpaka sasa matukio 198 ya maambukizi yamethibitishwa.

  Mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza kutoka Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa cha China Bw. Zeng Guang amesema mlipuko wa virusi hivyo vipya unaweza kudhibitiwa kama hatua zinachukuliwa sasa, kwa kuwa bado uko kwenye hatua ya mwanzo. Pia amekadiria kuwa idadi ya maambukizi inaweza kuongezeka zaidi katika msimu wa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina. Lakini ameeleza imani ya kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo, akisema mlipuko kama wa SARS uliotokea 2003 hautatokea tena.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako