• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mvua kubwa yasababisha vifo vya watu wanne kwenye Kusini mwa Msumbiji

    (GMT+08:00) 2020-01-21 09:50:57

    Mamlaka ya Msumbiji jana imeambia redio ya taifa ya RM kuwa, watu wanne wamekufa wikiendi iliyopita kutokana na mvua kubwa na upepo mkali ulioukumba mkoa wa kusini wa Maputo nchini humo.

    Mwakilishi kutoka Taasisi ya kitaifa ya Usimamizi wa Maafa (INGC) katika mkoa wa Maputo Bw. Rocha Nuvunga, amesema waathirika walikufa kwa radi, mafuriko na umeme kutokana na nyaya za umeme kuangushwa na upepo.

    Bw. Nuvunga amesema, matukio hayo yalitokea katika wilaya za Boane na Matola, ambapo nyumba zaidi ya 600 zilikuwa zimefurika maji. Pia ameongeza kuwa kazi za ukoaji zinaendelea ikiwemo kufungua vituo vya mpito kwa familia, ili kupunguza athari za hali mbaya ya hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako