• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi nane zaunga mkono kuanzisha tume ya usimamizi kwenye Mlangobahari wa Hormuz

    (GMT+08:00) 2020-01-21 10:12:17

    Wizara ya mambo ya Ulaya na mambo ya nje ya Ufaransa imetoa taarifa ya pamoja ikisema serikali za Ubelgiji, Denmark, Ufaransa, Ujerumani, Greece, Italia, Uholanzi and Ureno zimeahidi kuunga mkono kuanzishwa kwa tume ya usimamizi wa mambo ya majini inayoongozwa na Ulaya kwenye Mlangobahari wa Hormuz.

    Taarifa hiyo imesema hali ya hivi sasa huko eneo la Mashariki ya Kati inaleta wasiwasi mkubwa, ambayo imeongeza mvutano na uwezekano wa kutokea kwa mapambano makubwa, na kuiathiri vibaya eneo hilo. Eneo la Ghuba na Mlango bahari wa Hormuz linakumbwa na ukosefu wa usalama, hatua tulivu zinapaswa kuchukuliwa juu ya masuala hayo ya kiusalama.

    Taarifa hiyo imeongeza kuwa Tume ya usimamizi ya mambo ya majini ya Ulaya kwenye Mlangobahari wa Hormuz inalenga kuhakikisha hali ya usalama ya usafiri baharini, na kupunguza hali ya wasiwasi kwenye eneo hilo kwa kufuata sheria za kimataifa pamoja na makubaliano ya Umoja wa Mataifa juu ya sheria ya mambo ya bahari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako