• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Floyd Mayweather atangaza kutwangana na Conor McGregor na Khabib 2020

    (GMT+08:00) 2020-01-21 10:38:11

    Floyd Mayweather ameibuka na kuthibitisha kwamba atapambana na Conor McGregor na Khabib Nurmagomedov katika pambano la kurejeana mwaka huu. Nguli huyo wa ndondi kutoka Marekani alimshinda M-Ireland huyo huko Las Vegas Agosti 2017 katika pambano la raundi 10. Lakini kumekuwa na kelele kutoka kwa mashabiki wakitaka kuona pambano jingine la Mayweather, na bondia huyo amewasuuza moyo mashabiki wake baada ya kutoa tangazo hilo kwenye Instagram muda mchache tu baada ya McGrgeor kurejea tena ulingoni na kupata ushindi wa kishindo wa TKO kwa kumtwanga mpinzani wake Donald 'Cowboy' Cerrone kwa sekunde 40 tu. Bosi wa UFC Dana White amesema ni kweli kuhusu pambano hilo kwani mazungumzo yameshaanza. Wiki hii McGregor aliongea kuhusu azma yake ya kupambana tena na Mayweather.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako