• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China afanya ziara ya ukaguzi mjini Kunming

  (GMT+08:00) 2020-01-21 18:18:31

  Rais Xi Jinping wa China ameendelea na ziara ya ukaguzi mkoani Yunnan, na jana alikagua mji wa Kunming. Alitembelea Ziwa Dianchi, soko na Chuo Kikuu cha Ualimu cha Mkoa wa Yunnan ambacho kilikuwa Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Pamoja cha Kusini Magharibi wakati wa Vita Kuu yaPili ya Dunia.

  Ziwa Dianchi ni kituo cha kwanza cha ukaguzi wa Rais Xi. Likiwa ziwa kubwa zaidi la maji baridi mkoani Yunnan, Ziwa Dianchi lilikuwa chafu zaidi nchini China katika miaka ya 1990. Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na juhudi kubwa ya uhifadhi wa mazingira, maji ya ziwa hilo yamesafishwa kwa kiasi kikubwa. Rais Xi anasema,

  "Tunapaswa kuepuka njia ya zamani ya kuendeleza uchumi kwanza, na kushughulikia uchafuzi wa mazingira baadaye, na kuacha kabisa kitendo cha kuendeleza uchumi bila kujali uchafuzi wa mazingira. Wazo letu jipya la kujenga ustaarabu wa mazingira ya kiikolojia linaendana na utaratibu wa kiasili."

  Maonesho ya 14 ya bidhaa za sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina yanafanyika katika Jumba la Kimataifa la Mikutano la Kunming. Rais Xi alitembelea maonesho hayo ambapo alikuwa na haya ya kusema,

  "Hamjambo. Sikukuu ya mwaka mpya wa Panya inawadia, nawatakieni kila la heri wananchi wote wa China bara, Hong Kong, Macao na wengine walioko nje ya China. Nalitakia taifa letu kila la heri katika mwaka mpya. Pia nawatakieni wachina wa makabila mbalimbali kila la heri."

  Kituo cha mwisho cha ukaguzi wa Rais Xi mkoani Kunming ni Chuo Kikuu cha Uelimu cha Mkoa wa Yunnan ambacho kilikuwa Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Pamoja cha Kusini Magharibi wakati wa vita kuu ya pili duniani. Mwaka 1938, ili kuhifadhi chimbuko la elimu na utamaduni wa taifa la China, Chuo Kikuu cha Beijing, Chuo Kikuu cha Qinghua na Chuo Kikuu cha Nankai vilihamia katika mji wa Kunming ambao ulikuwa haujakaliwa na wavamizi wa Japan, na kuanzisha Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Pamoja cha Kusini Magharibi. Rais Xi anasema,

  "Wakati taifa letu lilipokabiliwa na tishio kubwa, wasomi na wanafunzi hodari wa China walikusanyika hapa, walifanikiwa hapa na walitawanya mbegu za elimu kila mahali. Watu waliofundishwa katika chuo hicho walitoa mchango muhimu katika zama tofauti za historia ya China. Hali hii inatuambia kuwa elimu inapaswa kuhusishwa kwa karibu na hatma na mustakabali wa taifa."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako