• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KEBS kusakak vipodozi hatari kote nchini

    (GMT+08:00) 2020-01-21 19:07:42

    Shirika la Kudhibiti Ubora wa Bidhaa Nchini (KEBS), litaongoza uchunguzi unaojumuisha taasisi mbalimbali kuhusu wafanyabiashara haramu wa kemikali za kugeuza rangi ya ngozi, wanaotengeneza mamilioni kwa kuuza vipodozi vilivyopigwa marufuku na kuhatarisha maisha ya Wakenya wengi.

    Wafanyabiashara hao hufanya ulanguzi wa bidhaa hizo kupitia mipaka isiyo na ulinzi mkali na kuziuza Nairobi na miji mingine katika biashara ya mamilioni inayostawishwa na wanawake wenye ngozi nyeusi na wenye kiu cha urembo.

    Mbinu mojawapo ya ulanguzi huo ni kuagizia bidhaa hizo nchini na kuzifanya kama zinazosafirishwa Congo lakini zinaachwa nchini huku njia nyingine ikitumia mabasi yanayopitia barabara ya Nairobi-Kinshasa, ambapo bidhaa hizo huingizwa Kenya.

    Mkurugenzi wa Kebs, Bw Bernard Njiraini, amesema kwamba kuongezeka kwa vipodozi haramu kumeibua wasiwasi ambao sasa utasababisha msako mkali unaolenga mabwenyenye wanaoagizia nchini vipodozi hivyo vilivyopigwa marufuku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako