• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Waganda na Watanzania wanapenda kutalii Kenya.

  (GMT+08:00) 2020-01-21 19:08:00

  Waganda na Watanzania wanaongoza kwa kutalii taifa la Kenya baada ya Wamarekani. Haya ni kwa mujibu wa ripoti maalum ya jinsi utalii unavyoendelea, ya mwaka wa 2019.

  Mwaka jana, Kenya ilipokea watalii 245,437 kutoka Amerika, hii ikiwa idadi ya juu zaidi kutoka taifa moja. Watalii wa Uganda waliozuru nchini Kenya ni 223,010 na wale wa kutoka Tanzania walikuwa 193,740.

  Watalii wa Uganda huenda wakaongezeka mwaka huu kutokana na kuanzishwa kwa safari za ndege za shirika la kitaifa la Uganda Airline, moja kwa moja kutoka Entebbe hadi uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi na uwanja wa Moi jijini Mombasa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako