• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa WEF asifu mafanikio yaliyopatikana na China katika kuondoa umaskini

    (GMT+08:00) 2020-01-21 19:09:19

    Rais wa Baraza la Uchumi wa Dunia WEF Bw. Borge Brende amesema, China imepata mafanikio makubwa katika kuondoa umaskini, na jumuiya ya kimataifa inapaswa kuunga mkono zaidi jitihada zake katika kusukuma mbele mfumo wa pande nyingi ili kupata maendeleo ya pamoja.

    Mada kuu ya mkutano wa baraza hilo kwa mwaka huu ni suala la malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa.

    Bw. Brende amesema, lengo kuu ni kuondoa umaskini kabla ya mwaka 2030, ambalo China imepata mafanikio makubwa katika historia ya binadamu kwa kuwaondoa Wachina milioni 800 kwenye umaskini uliokithiri. Pia amesema, ingawa China imeendelea kwa kasi sana, lakini baadhi ya maeneo bado ni maskini, hivyo China inahitaji kuendeleza juhudi hizo na kuzingatia zaidi usafi wa maji, hali ya hewa na kutoa ajira zaidi.

    Huu ni mwaka wa 50 tangu kuanzishwa kwa WEF. Mkutano wa mwaka huu wa WEF umekutanisha pamoja wanasiasa, wafanyabiashara na wajumbe kutoka jamii na sekta ya utamaduni kutafuta utatuzi wa masuala ya dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako