• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wuhan yaongeza udhibiti wa wasafiri wanaokwenda nje ya mji huo ili kuzuia kuenea kwa virusi

  (GMT+08:00) 2020-01-21 19:28:35

  Mji wa Wuchan, China umechukua hatua mfuluilizo kuongeza udhibiti na usimamizi wa wasafiri wanaokwenda nje ya mji huo, ikiwa ni juhudi za kuzuia kuenea kwa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya korona.

  Kwa mujibu wa kamati ya afya ya Wuhan, safari za makundi ya watalii za kwenda nje zimezuiliwa, na polisi wanayafanyia ukaguzi magari ya watu binafsi yanayotoka na kuingia mjini humo kama yanabeba ndege hai au wanyama pori. Vilevile vipimajoto zaidi ya 300 vinatumika kupima abiria wenye homa katika viwanja vya ndege, vituo vya treni, vituo vya mabasi na bandari za abiria.

  Abiria wenye homa wataandikishwa, kupewa barakoa na maelezo kuhusu homa ya mapafu na kushauriwa kukutana na madaktari. Kwa mujibu wa serikali ya mji huo, hakutakuwa na malipo yoyote kwa kufuta na kubadili tarehe za safari.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako