• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • IMF ina matarajio mazuri na mustakbali wa uchumi wa China

  (GMT+08:00) 2020-01-21 19:29:22

  Shirika la Fedha Duniani IMF limetoa ripoti likiongeza makadirio ya ukuaji wa uchumi wa China kwa mwaka huu hadi asilimia 6, na kupunguza yale ya uchumi wa dunia hadi asilimia 3.3 kwa mwaka huu na asilimia 3.4 kwa mwaka kesho.

  Akizungumzia hilo leo hapa Beijing, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Geng Shuang amesema, hii imeonyesha kuwa jamii ya kimataifa ina matarajio mazuri na imani na mustakbali wa uchumi wa China. Amesema ingawa changamoto za ndani na nje zinaongezeka, msingi wa maendeleo mazuri ya uchumi wa China kwa muda mrefu bado haujabadilika. Ameeleza kuwa, mwaka huu China itaendelea kuzifanyia mageuzi makubwa sekta za utoaji bidhaa na kutekeleza kwa ufanisi sera na hatua mbalimbali ili kuhakikisha uchumi wake unakua kwa kasi ya kuridhisha.

  Bw. Geng pia amesema toka mwaka jana, IMF imepunguza mara kadhaa makadirio yake na ukuaji wa uchumi wa dunia, jambo linaloashiria kuwa tatizo la kushuka kwa uchumi wa dunia bado halijapata ufumbuzi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako