• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China ni nchi ya pili kwa kupokea uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni mwaka jana

  (GMT+08:00) 2020-01-21 19:48:41

  Wizara ya biashara ya China leo imesema, China imeendelea kuwa nchi ya pili kwa kupokea uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni katika mwaka 2019, na uwekeaji huo umeongezeka kwa asilimia 5.8 ikilinganishwa na mwaka 2018 na kufikia dola za kimarekani bilioni 137.24.

  Naibu waziri wa biashara wa China Bw. Qian Keming amesema, makampuni mapya zaidi 40,000 yaliyowekezwa na nchi za nje yalianzishwa mwaka jana.

  Idadi ya miradi inayopokea uwekezaji wa moja kwa moja wenye thamani ya zaidi dola za kimarekani milioni 100 imefikia 834 katika mwaka 2019, ambayo iliongezeka kwa asilimia 15.8 kuliko mwaka 2018.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako