• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Yang Jiechi akutana na wenyeviti wa tume ya mazungumzo kati ya serikali kuhusu mageuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2020-01-21 21:28:33

    Mjumbe wa ofisi ya siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Yang Jiechi hapa Beijing amekutana na wenyeviti wa tume ya mazungumzo kati ya serikali kuhusu mageuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Lana Zaki Nusseibeh kutoka Falme za Kiarabu na Joanna Wronecka kutoka Poland.

    Yang amesema, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linabeba majukumu makuu ya kulinda amani na usalama duniani. Amesema lengo la mageuzi ya Baraza hilo ni kuongeza mamlaka na ufanisi wake, na kuongeza uwakilishi wa nchi zinazoendelea na nchi ndogo na zenye ukubwa wa kati. China itaunga mkono kazi za wenyeviti hao wawili, kuhakikisha mageuzi hayo yanasonga mbele kwa kufuata katiba ya Umoja wa Mataifa na maslahi ya pamoja ya nchi wanachama.

    Lana na Joanna wamesema wanatilia maanani msimamo na kazi ya China katika mageuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako