• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM wahimiza hatua za haraka zichukuliwe wakati nzige wa jangwani wanatishia usalama wa chakula katika Pembe ya Afrika

    (GMT+08:00) 2020-01-22 09:11:49

    Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limeonya kuwa makundi makubwa ya nzige wa jangwani yanaendelea kutishia usalama wa chakula katika Pembe ya Afrika.

    FAO imesema kutokana na kuwa hali ya hewa ya sasa katika Afrika Mashariki inatoa mazingira mazuri ya kuzaliana kwa nzige, idadi ya wadudu hao inaweza kuongezeka mara 500 kama hatua hazitachukuliwa.

    Shirika hilo pia limetahadharisha kuwa Sudan Kusini inakabiliwa na hatari kubwa ya uvamizi wa nzige wa jangwani wakati hali ya usalama wa chakula inazidi kuwa mbaya nchini humo.

    Mwakilishi wa FAO nchini Sudan Kusini amesema msaada wa dharura unahitajika kukabiliana na uvamizi wa nzige na kupunguza athari zake kwa usalama wa chakula.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako