• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bodi ya forodha ya Afrika Mashariki yapongeza reli ya SGR iliyojengwa na China

    (GMT+08:00) 2020-01-22 09:18:47

    Bodi ya forodha ya nchi za Afrika Mashariki imeipongeza reli ya SGR Mombasa-Nairobi-Naivasha kwa mchango wake katika kuboresha ufanisi wa ugavi.

    Mkuu wa Shirikisho la wasafirishaji wa mizigo la Afrika Mashariki Bw. Fred Seka amesema muda na gharama za kuagiza na kusafirisha nje mizigo vimepungua tangu kuzinduliwa kwa reli ya SGR. Amesema kwa sasa wafanyabiashara wa Rwanda, Uganda na Burundi wanaweza kuchukua mizigo yao Nairobi na Naivasha, badala ya Mombasa kama ilivyokuwa mwanzo.

    Bodi hiyo inasubiria kurefushwa kwa reli hiyo hadi magharibi mwa Kenya, na hatimaye Uganda na Rwanda.

    Bw. Seka amesema nchi za Afrika Mashariki zinatakiwa kuwekeza zaidi kwenye ujenzi wa reli ili kuboresha nguvu ya ushindani kwenye kanda hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako