• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa 39 wa Kamati ya wajumbe wa kudumu wa Umoja wa Afrika wafanyika Ethiopia

  (GMT+08:00) 2020-01-22 09:23:11

  Mkutano wa 39 wa Kamati ya wajumbe wa kudumu wa Umoja wa Afrika wenye mada ya "kutokomeza silaha" kujenga mazingira mazuri kwa ajili ya maendeleo ya Afrika" umefanyika kuanzia Januari 21 hadi 22 huko Addis Ababa, Ethiopia.

  Mabalozi wa nchi wanachama wa Umoja huo na maofisa wa nchi 55 wanachama wanatarajiwa kujadili rasimu ya ripoti na kuandaa ajenda ya Mkutano wa 36 wa Kamati tendaji ya Umoja huo, ambao utajumuisha mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama, uliopangwa kufanyika kuanzia Februari 6 hadi 7.

  Ajenda kuu ya mkutano huo ni kujadili mabadiliko ya kitaasisi ya Umoja huo na utekelezaji wa Mkataba wa Biashara Huru Katika Bara la Afrika (AfCFTA).

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako