• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasisitiza kutatuliwa kwa mgogoro wa Israel na Palestina kwa njia ya amani

    (GMT+08:00) 2020-01-22 09:40:35

    Mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuzihimiza Israel na Palestina zitatue mgogoro kati yao kwa njia ya mazungumzo ya usawa.

    Balozi Zhang amesema hayo katika Mjadala wa wazi wa robo mwaka katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Mashariki ya Kati likiwemo suala la Palestina, akiongeza kuwa Jumuiya ya kimataifa haswa pande husika za Mashariki ya Kati zinapaswa kufanya juhudi za pamoja kwa mujibu wa pendekezo la Amani la nchi za Kiarabu, kanuni ya amani kwa ardhi na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kuzihimiza Israel na Palestina kusuluhisha mgogoro kwa mazungumzo ya usawa.

    Habari nyingine zimesema jana usiku vikosi vya Israel viliwafyatulia risasi Wapalestina watatu wenye silaha waliotaka kuvuka kutoka Ukanda wa Gaza kuingia kwenye eneo la Israel.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako