• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maria Sharapova hatihati kutoka kwenye orodha ya wachezaji 350 baada ya kushindwa raundi ya kwanza

  (GMT+08:00) 2020-01-22 09:45:49

  Maria Sharapova hana uhakika kama atakuwepo kwenye michuano ya wazi ya Australia mwakani, baada ya kutolewa kwenye raundi ya kwanza ambayo ina maanisha atatoka kwenye wachezaji 350 bora duniani. Bingwa huyo wa mara tano wa Grand Slam, ambaye ameshinda Melbourne Park mwaka 2008, ameshindwa kwa 6-3 6-4 na Mcroatia Donna Vekic. Hiyo ni mara ya pili kwa Mrussia huyo kwenye mashindano tangu michuano ya wazi ya Marekani iliyofanyika Septemba kwasababu ya majeraha ya bega. Mchezaji huyo mwenye miaka 32 alipewa mwaliko kwenye mashindano hayo amesema amebahatika kuweza kufika hapo na kuwashukuru waandaaji kwa kumruhusu kushiriki mashindano haya na kwamba ni vigumu kwake kujua kitatokea nini katika miezi 12. Wakati huohuo mcheza tenisi namba moja duniani Rafael Nadal ameingia raundi ya pili ya michuano hiyo baada ya kumshinda Hugo Dellien kutoka Bolivia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako