Idara ya afya ya mji wa Wuhan, katikati ya China imetangaza kuwa mji huo umepanga vitanda 800 katika hospitali tatu na utatayarisha vingine 1200 katika muda mfupi ujao. Naibu mkurugenzi wa kamati ya afya ya mji Bw. Peng Houpeng amesema maeneo matano ya huduma maalumu yamewekwa kwenye hospitali tano za huko ambayo kila eneo linaangaliwa kwa ukaribu na wafanyakazi 30 wa matibabu siku zote.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |