• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu 440 wathibitishwa kuambukizwa virusi vipya vya korona nchini China

  (GMT+08:00) 2020-01-22 18:45:42

  Mamlaka ya afya ya China imetangaza kuwa, hadi kufikia Jumanne, watu 440 wamethibitishwa kuambukizwa na virusi vipya vya korona (2019-nCoV) vinavyoweza kusababisha ugonjwa wa nimonia katika mikoa 13 nchini humo.

  Naibu mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Afya ya China Bw. Li Bin amesema, hadi sasa watu tisa wamefariki kutokana na ugonjwa huo, na hao wote wanatokea mkoa wa Hubei. Nje ya China, kesi moja imethibitishwa nchini Japan, tatu nchini Thailand, na moja nchini Korea Kusini.

  Jumla ya watu 2,197 waliowasiliana kwa karibu na wagonjwa hao wamefuatiliwa, na kati yao, 1,394 bado wapo chini ya uchunguzi wa kiafya wakati wengine 765 wameondolewa. Bw. Li amesema, kesi za maambukizi zimekuwa zikiongezeka kwa haraka hivi karibuni, hali inayoweza kutokana na njia bora za utambuzi. Maambukizi kwa njia ya mfumo wa hewa ni njia kuu ya kuambukizwa virusi hivyo, na wataalam wametahadharisha kuwa kuna uwezekano wa virusi hivyo kubadilika, na hatari ya kuenea inaweza kuongezeka. Tangu Januari 20, China inmekuwa ikitoa ripoti kila siku kuhusu idadi ya kesi zilizothibitishwa na kesi zinazoshukiwa. Wataalam wametoa wito wa kuwa makini kwani watu wengi wanahama kati ya miji tofauti wakati wa sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina.

  Hatua kali zimechukuliwa ili kuzuia kuenea kwa virusi hivyo. Jumla ya vifaa 15 vya kutambua homa vimewekwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Tianhe mjini Wuhan, na vifaa vingine 20 vimewekwa katika vituo vitatu vya reli mjini humo. Bw. Li amesema, mji huo pia umeimarisha uchunguzi katika masoko ya wakulima, maduka makubwa na migahawa, na kukataza biashara ya wanyama pori. Aidha, mikusanyiko ya watu itazuiliwa, na safari zisizo za lazima kati ya mji wa Wuhan na sehemu nyingine pia zitadhibitiwa, ili virusi visienee zaidi nje ya mji huo. Mkuu wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha China Bw. Gao Fu amesema, kufuatia ushahidi wa sasa, virusi hivyo vilitokana na wanyama pori iliyouzwa katika soko la vyakula vya baharini la Wuhan. China imebadilishana taarifa mara 15 na Shirika la Afya Duniani (WHO), Hong Kong, Macao, Taiwan na nchi za nje zinazohusika, licha ya hayo, Tume ya Taifa ya Afya ya China imekutana mara nne na wataalamu wa WHO, na kuwaalika kutembelea Wuhan ili kupata habari ya moja kwa moja.

  Aidha, Bw. Li amesema, China imedumisha mawasiliano ya karibu na ubalozi na idara husika za Thailand, Japan, Korea Kusini, Marekani na nchi nyinginezo nchini China, ili kutoa habari mpya, na kuzisaidia kukagua na kutambua virusi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako