• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lapongeza matokeo ya Mkutano wa Berlin kuhusu Libya

  (GMT+08:00) 2020-01-22 19:28:27

  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepongeza matokeo ya mkutano wa kimataifa kuhusu Libya uliofanyika jana mjini Berlin.

  Balozi wa Vietnam kwenye Umoja wa Mataifa Dang Dinh Quy, ambaye nchi yake ni mwenyekiti wa zamu wa Baraza hilo kwa mwezi Januari, amesema Baraza hilo litakuwa na majadiliano zaidi katika siku za baadaye ili kufuatilia hitimisho la mkutano wa Berlin. Pia amesema, nchi wajumbe wa Baraza hilo wamesisitiza kumuunga mkono mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Ghassan Salame na juhudi zake za kusimamisha vita, na ufumbuzi wa kisiasa unamilikiwa na kuongozwa na watu wa Libya. Ameongeza kuwa nchi wajumbe wa Baraza hilo pia wamezihimiza pande zinazohusika nchini Libya kufikia makubaliano ya kusimamisha vita haraka iwezekanavyo.

  Naye katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyehudhuria mkutano wa Berlin ametoa wito wa mchakato halisi wa kisiasa baada ya makubaliano ya kusimamisha vita kufikiwa nchini Libya. Amesema mkutano huo ulikuwa ni hatua kubwa, lakini bado kuna safari ndefu katika siku za baadaye.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako