• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanafunzi waliotekwa nyara nchini Cameroon waokolewa

  (GMT+08:00) 2020-01-22 19:28:47

  Jeshi la Cameroon limewaokoa wanafunzi 24 waliokuwa wakishikiliwa na waasi wenye silaha katika eneo linalozungumza Kiingereza la Meme nchini humo.

  Ofisa mwandamizi wa eneo hilo Ntou Ndong Chamberlain amesema, watoto hao walitekwa nyara mapema Jumanne kwenye shule yao iliyopo kusini magharibi mwa mji wa Kumba na kupelekwa katika msitu ambako kuna kambi ya waasi. Waasi wawili waliuawa kwa risasi katika operesheni ya uokoaji, na silaha na risasi zimekamatwa.

  Watoto hao wenye umri wa miaka mitano hadi 10 wamerudishwa kwenye familia zao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako