• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaongeza nguvu za utekelezaji sheria na ulinzi wa hakimiliki za ubunifu

  (GMT+08:00) 2020-01-22 19:49:55

  Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Geng Shuang amesema, China imeongeza nguvu za utekelezaji sheria na ulinzi wa hakimiliki za ubunifu, na kuahidi kuzitendea kwa usawa kampuni za ndani na nje ya China.

  Geng amesema hayo alipozungumzia ripoti iliyotolewa hivi karibuni na gazeti la Financial Times ikisema, ulinzi wa hakimiliki hizo unaimarishwa nchini China na kuifanya nchi hiyo iwe nchi ya ubunifu. Takwimu zinaonesha kuwa, hivi sasa China inachukua nafasi ya pili duniani kwa kutenga fedha katika utafiti na maendeleo, na kuongoza duniani kwa kutoa maombi mengi ya hataza. Wakati huohuo, kwa mujibu wa Shirika la Hakimiliki ya Ubunifu Duniani WIPO, mwaka jana, China ilishika nafasi ya 14 duniani katika mambo ya ubunifu.

  Hata hivyo, Bw. Geng amekiri kuwa China bado ni nchi inayoendelea, na ulinzi wa hakimiliki ya ubunifu una mapungufu, lakini itajitahidi kuinua uwezo wa kubuni, kutumia, kulinda na kuhudumia hakimiliki hiyo. Pia amesema, China imejiunga na karibu mikataba yote ya kimataifa kuhusu hakimiliki ya ubunifu na imeanza mchakato wa ndani wa kisheria kwa ajili ya kujiunga na Mkataba wa Hague kuhusu Usajili wa Kimataifa wa Ubunifu wa Bidhaa za Kiviwanda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako