• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Baraza la Seneti la Marekani lapitisha pendekezo la azimio la Republican la kanuni za kesi dhidi ya rais wa nchi hiyo

  (GMT+08:00) 2020-01-22 19:51:13

  Baraza la Seneti la Marekani mapema leo limepiga kura na kupitisha pendekezo la chama cha Republican la kuweka kanuni za kuongoza kesi inayoendelea dhidi ya rais Donald Trump, na kuondoa marekebisho 11 yaliyopendekezwa na chama cha Democrats.

  Azimio hilo limefikiwa kwa kura 57 kwa 43 katika baraza la Seneti ambalo lina wanachama wengi kutoka chama cha Republican, na litaahirisha uamuzi wa kama kuita mashahidi zaidi mpaka utetezi wa awali wa pande zote mbili utakaposikilizwa.

  Suala la mashahidi lilikuwa ni ufunguo muhimu uliowafanya wasimamizi wa Ikulu ya nchi hiyo kubadilishana maneno kwa zaidi ya saa 12.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako