• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uhusiano kati ya Botswana na China unalenga kuondoa umasikini na upatikanaji wa ajira

  (GMT+08:00) 2020-01-22 20:18:54

  Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Botswana na China umeendelea kuwa na kuongozwa na malengo ya maendeleo ya binadamu, kuondoa umasikini na kutoa nafasi za ajira.

  Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Botswana, Unity Dow, amesema hayo katika hafla ya kutimiza miaka 45 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hiyo na China iliyofanyika Gaborone.

  Amesema hafal hiyo imeashiria hatua kubwa ya kihistoria ya uhusiano wa muda mrefu, wa kina na endelevu kati ya nchi hizo mbili, ambao pia umeendelea kustawi kutokana na msingi imara wa kuelewana, kuheshimiana, na kuaminiana.

  Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na jamii ya Wachina wanaoishi na kufanya kazi nchini Botswana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako