• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalam wa WHO watembelea Wuhan kukagua kazi zinazohusiana na mlipuko wa virusi vipya vya Korona

    (GMT+08:00) 2020-01-22 20:19:32

    Kamati ya Taifa ya Afya ya China imesema, kundi la wataalam kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) wametembelea mji wa Wuhan, mkoa wa Hubei, jumatatu na jumanne wiki hii kukagua kazi zinazohusiana na mlipuko wa nimonia inayosababishwa na maambukizi ya virusi vipya vya korona.

    Wataalam hao walikagua vifaa vya kupima joto la mwili kwa wasafiri wanaotoka nje ya mji huo katika uwanja wa ndege na bandari, ambapo maambukizi ya mwanzo ya ugonjwa huo yaliripotiwa. Pia walifuatilia utaratibu mzima wa kupima, kuweka karantini, na tiba kwa wagonjwa wenye homa kwenye hospitali moja mjini humo na kutembelea maabara ya Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Mkoa wa Hubei.

    Wataalam hao wameeleza kuridhishwa na jinsi China inavyotoa taarifa kwa hiari juu ya mlipuko huo, kueleza jinsi virusi hivyo vinavyobadilika, na kuwa tayari kubadilishana taarifa za jinsi ya kuzuia, kudhibiti na mpango wa matibabu kwa ajili ya siku zijazo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako