• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China azungumza na viongozi wa Ufaransa na Ujerumani kwa njia ya simu

  (GMT+08:00) 2020-01-22 20:19:59

  Wakati Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina ikikaribia, rais Xi Jinping wa China amezungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron na chasela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel kwa nyakati tofauti.

  Alipozungumza na rais Macron, rais Xi amesema mwaka jana uhusiano kati ya China na Ufaransa umeendelea kwa kiwango cha juu, na mwaka huu China inapenda kushirikiana na Ufaransa kuhakikisha uhusiano huo unaendelea zaidi. Aidha, rais Xi amesema huu ni mwaka wa 45 tangu China na Umoja wa Ulaya kuanzisha uhusiano rasmi, na kutaka pande hizo mbili zifikie makubaliano ya uwekezaji ya kiwango cha juu, kulinda utaratibu wa pande nyingi, na kulinda biashara huria. Pia kukamilisha usimamizi wa mambo ya kimataifa, kujenga kwa pamoja uchumi wa dunia unaofungua mlango, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na kuhimiza uhusiano kati yao uwe na kiwango cha juu zaidi.

  Rais Macron ameeleza matumaini yake kwamba, nchi hizo zitaendelea kusukuma mbele ushirikiano katika biashara, uwekezaji na uhifadhi wa mazingira.

  Alipogunzumza na Bibi Merkel, rais Xi amesema China siku zote inatilia maanani uhusiano kati yake na Ujerumani, na kupenda nchi hizo zitakuwa washiriki wa kutegemeana.

  Bibi Merkel amesema nchi yake inataka kudumisha mazungumzo na mawasiliano na China katika ngazi tofauti, na kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako