• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ukosefu unaozidi wa usawa wazuia maendeleo ya uchumi na jamii

  (GMT+08:00) 2020-01-22 22:27:18

  Ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa jana imesema, ukosefu unaozidi wa usawa kwenye nchi zinazoendelea na nchi zilizoendelea inaweza kuzidisha pengo na kuzuia maendeleo ya uchumi na jamii.

  Kutokana na ripoti ya jamii ya dunia ya mwaka 2020, zaidi ya theluthi mbili ya watu wa dunia wanaishi kwenye nchi ambapo ukosefu wa usawa umeongezeka kuanzia mwaka 1990, aidha ukosefu wa usawa unaongezeka tena hata katika baadhi ya nchi ambazo zimeshuhudia kupungua kwa ukosefu wa usawa katika miaka zaidi ya 10 iliyopita.

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema, ripoti hiyo imetolewa wakati dunia inakabiliwa na hali ngumu ya ukosefu wa usawa duniani. Tofauti ya mapato na ukosefu wa fursa vinasababisha ukosefu wa usawa, kukatisha tamaa na kutoridhika kwa vizazi vyote.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako