• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yashikilia njia sahihi ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na maendeleo endelevu

    (GMT+08:00) 2020-01-22 22:27:39

    Mkutano wa mwaka 2020 wa baraza la uchumi la dunia unafanyika kuanzia tarehe 21 hadi tarehe 24 huko Davos nchini Uswiss.

    Akizungumza na wanahabari, Mkurugenzi mkuu wa baraza hilo Bw. Borge Brede amesema, China inashikilia njia sahihi ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kutimiza maendeleo endelevu.

    Pia amesema, ingawa kupunguza utoaji wa hewa chafu ni changamoto kubwa kwa China inayohimiza maendeleo ya uchumi, lakini nchi hiyo inafanya juhudi kutekeleza makubaliano ya Paris na kutenganisha ongezeko la uchumi na utoaji wa hewa chafu. Aidha amesema China ilitoa mchango mkubwa ambao nishati ya jua inatumika kwa kiwango kikubwa.

    Bw. Brende amekubaliana na mawazo ya viongozi wa China kwamba haiwezekani kutozingatia mazingira kwa kuhimiza maendeleo ya uchumi, akiamini kuwa uchumi wa China utazingatia uhifadhi wa mazingira na maendeleo ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako