• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kizee wa miaka 74 asajiliwa na timu ya 6th October FC nchini Misri

  (GMT+08:00) 2020-01-23 09:30:00

  Shirikisho la Soka la Misri (EFA) limetangaza kupokea usajili wa mchezaji mzee zaidi katika historia ya soka ya kulipwa duniani. Klabu ya daraja la tatu ya 6th October FC imemsajili Eez Eldin Bahder akiwa babu wa umri miaka 74, akitarajia kuanza kuichezea timu hiyo hivi karibuni. Hakuna taarifa ya ziada iliyotolewa kuhusu mkataba wa Bahder na klabu hiyo. Babu huyo hajulikani katika rekodi za wachezaji wa soka Misri kwa sababu hakuna klabu yoyote kubwa aliyowahi kuichezea. Hivyo EFA na Badher imewakaribisha Guinness Book of World Records kwenda kushuhudia mechi ya daraja la tatu ili kuona babu huyo akicheza soka yake ya kulipwa akiwa na umri mkubwa zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako