• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maseneta wa Democrats watoa maelezo ya ufunguzi kwenye kesi dhidi ya Rais Trump

  (GMT+08:00) 2020-01-23 09:47:21

  Kundi la wajumbe saba wa chama cha Democrats wakiwa kama ni waendesha mashtaka, wameanza kutoa maelezo ya ufunguzi kwenye baraza la seneti wakieleza ni kwanini rais Trump ashitakiwe na kuondolewa madarakani, wakati kesi yake imeanza kusikilizwa.

  Mwenyekiti wa kamati ya usalama Bw. Adam Schiff anayeongoza uchunguzi ametoa hoja zake kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na baraza la chini la bunge la Marekani, kuhusu shughuli za Rais Trump kwa Ukraine na kupuuza madaraka ya baraza hilo kuchunguza makosa yanayostahili aondolewe madarakani, na kusema Rais Trump anatakiwa kushitakiwa na kuondolewa madarakani.

  Amesema kama Trump hatachunguzwa na kuondolewa madarakani kutokana na kutumia madaraka yake vibaya na kuliingilia baraza la seneti, basi marais wajao watafanya kazi kama wasioweza kuwajibishwa, kusimamiwa na bunge, na kuwa juu ya sheria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako