• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mji wa Wuhan wasimamisha usafiri wa umma, safari za ndege na treni za kutoka

  (GMT+08:00) 2020-01-23 09:58:35

  Mamlaka ya Wuhan imetangaza kusimamisha usafiri wa umma na kufunga uwanja wa ndege na vituo vya reli kwa abiria wanakaoondoka Wuhan, huku ikipendekeza wakazi kutoondoka kutoka mji huo isipokuwa wakiwa na sababu maalumu.

  Habari kutoka makao makuu ya udhibiti na matibabu ya virusi vipya vya nimonia aina ya 2019-nCoV zinasema hatua hiyo inatekelezwa kuanzia saa 4 asubuhi ya tarehe 23 hadi taarifa mpya zitakapotolewa.

  Hadi saa 6 alfajiri ya tarehe 23, watu 571 walithibitishwa kuambukizwa virusi hivyo kote nchini, na wengine 17 wamefariki dunia ambao wote ni wa mji wa Wuhan.

  Waliothibitishwa kuambukizwa virusi hivyo nje ya China bara ni pamoja na mtu mmoja Hongkong, Macao, Taiwan, Marekani, Japan, Korea Kusini na watatu nchini Thailand.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako