• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa asema binadamu wanakabiliwa na matishio makuu manne

  (GMT+08:00) 2020-01-23 10:17:18

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York kwamba sasa binadamu wanakabiliwa na matishio makuu manne ambayo yanaweza kuhatarisha maendeleo katika karne ya 21.

  Bw. Guterres amesema hayo akitoa ripoti isiyo rasmi kwenye Mkutano Mkuu wa UM, kujumlisha vipaumbele vyake kwa mwaka 2020. Matishio hayo manne ni mivutano kimkakati ya dunia isiyoonekana katika miaka mingi iliyopita, msukosuko wa mabadiliko ya hali ya hewa, ongezeko la kutoaminiana kwa dunia, athari mbaya za teknolojia ya dijitali.

  Bw. Guterres ametoa wito watu wa duniani kote kushiriki katika mazungumzo ya kimataifa yaliyoanzishwa na Umoja wa Mataifa kujadili jukumu la ushirikiano wa kimataifa katika kujenga mustakbali tunaotaka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako