• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la umeme la Zambia lakanusha kusimama kwa ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme

    (GMT+08:00) 2020-01-23 10:56:55

    Shirika la umeme la Zambia limekanusha ripoti kuwa kazi za ujenzi wa kituo kikubwa cha umeme kinachotarajiwa kuhimiza uzalishaji wa umeme zinaweza kusimamishwa kutokana na matatizo ya kifedha.

    Ripoti kutoka baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa zimeonesha kuwa ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya maji cha bwawa la Kafue chenye thamani ya dola bilioni 2 za kimarekani kilichoko kusini mwa Zambia, unaweza kusimamishwa baada ya shirika la umeme la Zesco kushindwa kuhakikisha utoaji wa fedha.

    Msemaji wa shirika hilo Bw. Henry Kapata amesema ripoti hizo zinapaswa kuondolewa, kwa sababu zote ni za uwongo huku akiongeza kuwa ujenzi wa kituo hicho unaendelea vizuri na hakuna tatizo lolote la kifedha linaloathiri kazi za ujenzi.

    Kwa mujibu wa msemaji huyo maofisa wa serikali pamoja na maofisa wa shirika hilo wametembelea kituo hicho na kukagua mchakato, na ripoti kuhusu kusimama kwa ujenzi wa kituo hicho ni sehemu ya habari za uwongo kutoka kwenye mitandao ya kijamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako